RAHA TELE:- Picha 5 wakati Taifa Stars ya Tanzania itakata Uwanja wa Taifa leo October 12,2014 dhidi ya Benin na kuwatungua 4-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 12, 2014

RAHA TELE:- Picha 5 wakati Taifa Stars ya Tanzania itakata Uwanja wa Taifa leo October 12,2014 dhidi ya Benin na kuwatungua 4-1.

Jukwaani ni Washabiki wa Taifa stars wakiisapoti vilivyo timu yao....Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi mnono dhidi ya  Benin wa mabao 4-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa Kalenda ya FIFA leo October 12,2014,jioni katika  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo ,Taifa  Stars  hadi Mapumziko tayari ilikuwa inaongoza mabao 2-0,kwa mabao ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16 na kiungo Amri Kiemba dakika ya 39.

Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars,Juma Luizio akiipachikia bao la nne kwa timu yake katika mtangange wa kikataifa wa kirafiki dhidi ya Benin, katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu aliifungia Taifa Stars bao la tatu dakika ya 49 akimalizia krosi fupi ya Mrisho Ngassa aliyemtoka vizuri beki wa Benin.

Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia, Juma Luizio aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Ngassa, aliifungia Stars bao la nne akimalizia kazi nzuri ya Ulimwengu aliyemtoka beki wa Benin.

Benin ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Suanon Fadel dakika ya 90.
 Wachezaji wa Taifa Stars,wakishangilia ushindi wao huku wakiwaacha wapinzani wao wa Benin wakiwa hoi tena wakiwa hawaamini wanachokiona uwanjani hapo.


Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad