LIGI SOKA WILAYA YA NGARA:- Haya ndio Matokeo ya mechi zilizochezwa October 10,2014 na Msimamo wa Kila kundi . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 11, 2014

LIGI SOKA WILAYA YA NGARA:- Haya ndio Matokeo ya mechi zilizochezwa October 10,2014 na Msimamo wa Kila kundi .


Pichani ni Timu ya Kabanga FC wakichuana na Mabawe FC kwenye uwanja wa Kokoto wakati wa Mchezo wa Ligi ngazi ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera 2014/2015 hapo October 10,2014.

 Ligi soka  wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeendelea tena October 10,2014 katika viwanja viatu tofauti vilivyopangwa kuchezewa mechi hizo. 

Katika uwanja wa Rulenge timu ya Rulenge White Stars imeiadhibu timu ya Nyakisasa FC kwa jumla ya goli 9 -1 na hivyo kujihakikishia kufuzu hatua ya Robo fainali kutoka kundi lao la C lenye Ngara Stars ambao watakao kamilisha ratiba ya kundi hilo October 12,2014 dhidi ya Nyakisasa FC.

Katika uwanja wa Benaco,Timu ya Ngara Boys FC imeilaza timu ya Rusumo FC kwa goli 1 - 0. 

Katika kundi hili la B,hapo kesho October 12,2014,Benaco Stars watahitaji kujihakikishia ushindi dhidi ya Rusumo FC ili kufuzu hatua ya Robo fainali kwani katika kundi lao lenye Rusumo FC na Ngara Boys FC kila timu inanafasi ya kusonga mbele.

Na katika uwanja wa Kokoto mjini Ngara, Timu ya Kabanga FC  imejihakikishia kufuzu hatua ijayo baada ya kuilaza timu ya Mabawe FC kwa goli 3 -  2 na hivyo kufikisha Pointi 4.

Mechi za kundi hili la A zinakamilishwa October 12,2014,kwa Walimu FC pale watakapo shuka dimbani kutafuta ushindi ili ifuzu dhidi ya Mabawe FC.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

RATIBA / MATOKEO YA MASHINDANO LIGI SOKA WILAYA YA NGARA 2014/2015.
UWANJA
TIMU
TAREHE
KOKOTO
KABANGA 1-1 WALIMU
8/10/2014
KOKOTO
MABAWE 1-3 KABANGA
10/10/2014
KOKOTO
WALIMU v  MABAWE
12/10/2014
BENACO
BENACO 2-1 NGARA BOYS
8/10/2014
BENACO
NGARA BOYS 1 - 0 RUSUMO FC
10/10/2014
BENACO
RUSUMO v BENACO
12/10/2014
RULENGE
RULENGE 1-1 NGARA STARS
8/10/2014
RULENGE
NYAKISASA 1 - 9 RULENGE
10/10/2014
RULENGE
NGARA STARS v NYAKISASA
12/10/2014

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad