PICHA / AJALI YA MTUMBI KIGOMA:- Watu 10 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 13, 2014

PICHA / AJALI YA MTUMBI KIGOMA:- Watu 10 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa.

Hadi waokoaji wana ahirisha zoezi kwa jana October 12,2014, ili kurejea tena leo October 13,2014,Jumla ya maiti 7 zimeopolewa hivyo kufikisha maiti 10 . Hata hivyo imeelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ,Luten Kanali Mstaafu Issa Machibya bado miili mingi haijafikiwa.

Watu 10 wamekufa  na 27 wameokolewa na wengine 11 kulazwa katika hospitali ya rufaa maweni iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma baada ya boti walilokuwa wakisafiria kuzama juzi October 11,2014, katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari,Kamishina msaidizi wa Polisi mkoa,Kamanda Jafar Mohamed amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 9 Mchana katika kijiji cha Kalalangabo kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika kwenye halmashauri ya wilaya Kigoma.

Kamanda Mohamed amesema chanzo cha tukio hilo ni idadi kubwa ya watu waliokuwa katika boti hilo na kusababisha kuzama majini mita 200 kutoka nchi kavu na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye sherehe ya harusi katika kijiji cha Kigalye kilichopo jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani humo.

Kamanda amesema hatua za uokoaji zinaendelea sanjari na taratibu za kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma inayowakabili.
Zoezi hilo la kuwatafuta watu wengine linafanywa na wavuvi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Ndugu,Jamaa na Wapambe wa Bwana na Bibi Harusi walionusurika kifo baada ya ajali ya mtumbwi kutokea katika kijiji cha kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma.
Bibi harusi, Mariamu Juma (18) aliyenusurika kifo katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa naendelea na matibabu katika hospital ya  mkoa wa Kigoma,amesema chanzo ni baada ya mitubwi hiyo kukumbwa na wimbi la maji sambamba na idadi kubwa ya watu ambao walikuwa katika mitumbwi hiyo.
Mitumbwi iliyosababisha ajali ilikuwa miwili ambayo ni maalum kwa kuvulia samaki na dagaa hivyo ilitumika kusafirishia abiria baada ya kukodiwa kwa lengo la kuwfikisha maharusi katika kijiji cha Kigalye wakitokea katika kijiji cha Mwandiga jimbo la Kigoma Kaskazini ndipo walipokutwa na janga hilo.

Inaelezwa kuwa,kuzama kwa mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watu waliokuwa katika magari matatu aina ya Hiace pamoja bodaboda tatu kiasi ambacho kinaashiria watu hao walikuwa wengi ukilinganisha na uwezo wa mitumbwi hiyo ambayo hubeba watu 20 tu wakati wa shughuli za uvuvi.

Pia inaelezwa kuwa eneo ambalo walitumia kupakia abiria hao ilikuwa katika kijiji cha Kalalangabo ambapo si rasmi kwa kupakia abiria kisheria na hivyo kutakiwa kutumia eneo la kibirizi ambalo limetengwa kisheria.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad