AJALI :-Cheki Picha hizi 5 za Lori likianguka kisa kuteleza kutokana na mvua iliyonyesha Leo October 12,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 12, 2014

AJALI :-Cheki Picha hizi 5 za Lori likianguka kisa kuteleza kutokana na mvua iliyonyesha Leo October 12,2014.

Lori aina ya Scania namba T 607 CWV Semi Taller (kama linavyoonekana katika picha) lililokuwa limebeba kokoto limeanguka katikati ya Barabara leo October 12,2014, katika eneo la Chalinze Mzee Mkoani Pwani na kuharibika vibaya.

Kwa  mujibu wa Mashuhuda, ajali hiyo ametokea baada ya gari hilo lililokuwa likielekea Dar es Salaam, kuteleza kutokana na mvua iliyonyesha asubuhi ya leo mkoani humo.

Hata hivyo askari wa usalama barabarani walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuliondoa gari hilo ambalo limesababisha foleni kubwa ya magari yaliyokuwa yakitokea jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na kuziba barabara.



Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad