Msanii wa
Bongo Fleva, Ali Kiba akipafomu.
TIFU
LILIVYOKUWA.
Kwenye shoo
hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni
jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba),
walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.
|
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
CHANZO
CHANENA
Chanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani. |
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
akifanya shoo na Davido wa Nigeria.
“Ishu
ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi, wakajipanga katika maeneo
tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza
vizuri azma yao ya kuharibu pindi Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai
chanzo hicho.
WALIFANIKIWA?
Kwa namna moja mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond ashtukie na kuamua kutamka hadharani: “Jamani kuna uhuni unaendelea hapa.” |
Mkurugenzi wa Times FM, Rehure Nyaulawa.
TEAM
DIAMOND WACHARUKA
Madai yanasema mara baada ya Team Kiba kufanya vurugu hizo na kufanikiwa, baadhi ya mashabiki ambao waliaminika ni wa Diamond (Team Diamond), walicharuka na kusema hawakubaliani na uhuni huo ambao umefanywa hivyo watahakikisha wanapambana kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile. “Hatukubali, wao si walijipanga hapa kumharibia Diamond, sasa na sisi tutahakikisha tunalipiza kisasi kwa namna yoyote,” walisikika wakisema mashabiki wa Diamond.
TALE
AKIRI KUSIKIA
Paparazi wetu aliwatafuta Diamond na Kiba ili kujua wanazungumziaje vurugu hizo. Baada ya kumtafuta Diamond bila mafanikio, alipatikana meneja wake, Hamis Taletale ‘Bab Tale’ ambaye alikiri kuwepo kwa maandalizi ya zomeazomea ambayo yalikuwa na lengo ya kumharibia msanii wake. |
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media
Group, Ruge Mtahaba.
“Hizi kwetu
tumezichukulia kama changamoto, tulisikia kwamba kuna watu wamelipwa kwa ajili
ya kufanya fujo lakini hatukujali sana kwani lengo letu si kugombana na mtu,
sisi tunafanya muziki mzuri ambao ndoto zetu ni kuufikisha katika levo za
Kimataifa,” alisema Bab Tale.
KIBA
ANAHUSIKA?
Alipotafutwa Kiba kuzungumzia suala hilo alikataa kuhusika nalo na kudai halina ukweli wowote kwani si rahisi kuwalipa pesa mashabiki wengi kiasi kile waliojitokeza uwanjani. “Hiyo si kweli ni uzushi tu, sasa mimi nitawalipa nini hao mashabiki wote waweze kumzomea huyo Diamond? Siyo rahisi. Kwanza mimi nifanye hivyo ili iweje? Mimi si mtu wa kushindana na Diamond hata siku moja, nafanya muziki wangu, mashabiki wanauelewa, nashukuru Mungu kwa hilo,” alisema Kiba.
CLOUDS FM
VS TIMES FM
Kwa upande mwingine, vita nzito ilizidi kutokota kupitia tamasha hilo baada ya msanii Davido kupanda jukwaani na kutumbuiza ilhali akiwa amewekewa pingamizi la kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) sambamba na zuio la Mahakama ya Kisutu lililowekwa na Redio Times FM waliodai kuwa na mkataba wa kufanya shoo na msanii huyo Novemba, mwaka huu Bongo.
TIMES
WANASEMAJE?
Mkurugenzi wa Redio Times FM, Rehure Nyaulawa alipotafutwa kwa simu kuhusiana na suala hilo alisema mahakama ilishaweka pingamizi, anashangaa kuona msanii huyo alipanda jukwaani lakini akasema hawezi kukaa kimya, atakwenda mbele zaidi ili haki itendeke.
CLOUDS
JE?
Kwa upande wao, Clouds walipotafutwa hawakupatikana hewani lakini kimsingi na wao wana hoja zao ambazo zitabainika pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Hata hivyo,
kuna madai kwamba, zuio la Davido kutopanda jukwaani Leaders Club lilipelekwa
na mahakama kwa Clouds Media Group wakati Tamasha la Fiesta linaandaliwa na
Kampuni ya Primetime Promotion, kwa hiyo barua hiyo ilikuwa ‘missing in
action’.
Stori:-
Erick Evarist, Musa Mateja na Chande Abdallah/GBL.
Karibu
kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana
/Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment