MSIBA MWINGINE TENA LEO OCTOBER 21,2014:- Baada ya YP, tumeondokewa na Uuigizaji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 21, 2014

MSIBA MWINGINE TENA LEO OCTOBER 21,2014:- Baada ya YP, tumeondokewa na Uuigizaji.

Ni masaa machache tu yamepita tangu muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bongo Fleva kumpoteza aliyekuwa staa wa muziki huo kutoka kundi la TMK Wanaume Family, aliyekuwa akifahamika kwa jina la YP, taarifa nyingine ya simanzi inahusu msiba wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Muvi.

Katika ukurasa wake wa instagram, Muigizaji na mchekeshaji maarufu anayefahamika kwa jina la Kitale ama Mkude Simba (@mkudesimbaoriginal), amepost picha ya muigizaji Shery Mwana aliyefariki masaa machache yaliyopita pia.

Kwa mujibu wa Kitale, muigizaji huyo mbaye jina lake halisi ni Sherry Charles Magali, aliwahi kushiriki na Kitale katika movie mbali mbali ikiwemo ya ‘Kipotabo’ na ‘Nyumba Nne’.


Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa leo October 21, 2014, katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.

Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema “Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali

Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”

Mwanawamakonda Blog inatoa pole kwa familia ya Yesaya Ambilikile YP, Wadau wa Muziki,Ndugu ,Jamaa na Marafiki, ((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu))
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad