MAENDELEO:-Yaliyojiri kwa Picha wakati Rais Kikwete akizindua Daraja la Waenda kwa miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza October 10,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 11, 2014

MAENDELEO:-Yaliyojiri kwa Picha wakati Rais Kikwete akizindua Daraja la Waenda kwa miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza October 10,2014.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi daraja la waenda kwa miguu eneo la Mabatini Mkoani Mwanza Octoba 10,2014.

Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli.Rais Jakaya Kikwete amezindua daraja la waenda kwa miguu katika eneo la Mabatini jijini Mwanza na kuliagiza jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani mara moja baadhi ya watu wakiwemo waendesha pikipiki wanaokiuka matumizi ya daraja hilo.

Daraja hilo la kwanza na la aina yake kujengwa hapa nchini limegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 800, mbali na kupunguza msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Mwanza- Musoma, pia limesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali takribani nane za waenda kwa mguu zilizokuwa zikitokea kila mwezi ambapo watu wawili walikuwa wakipoteza maisha papo hapo.
Muonekano wa Daraja la waenda kwa miguu liliojengwa eneo la Mabatini Jijini Mwanza lililozinduliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Octoba 10,2014. (Picha na Freddy Maro)

Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimuongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kukagua daraja la waenda kwa miguu huko Mabatini Mkoani Mwanza  muda mfupi baada ya kulifungua Octoba 10,2014.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua daraja la Nyashishi lenye urefu wa mita 67 lililopo katika barabara ya Usagara Kisesa wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara kilometa 16 ya  Kisesa hadi Usagara inayojengwa kwa kiwango cha lami Octoba 10,2014
Aidha, Rais Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kisesa – Usagara inayojengwa na mkandarasi kampuni ya Nyanza Road Contruction kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 16 kwa gharama ya shilingi bilioni 19.94 na kupiga marufuku malori ya mizigo kutoka nchi jirani ya Kenya na mkoa wa Mara kuendelea kuingia jijini Mwanza pindi barabara hiyo itakapokamilika.

Awali waziri wa ujenzi Mh.John Pombe Magufuli ameeleza kukerwa na tabia ya baadhi ya watu walioanza kugeuza matumizi ya daraja hilo la waenda kwa miguu kwa kupanda juu yake nyakati za usiku na kuponda magari kwa mawe pamoja na kuhujumu miundombinu ya daraja hilo, huku mbunge wa jimbo la Nyamagana Mh. Ezekiel Wenje akiiomba wizara ya ujenzi kujenga barabara ya Igoma –Buhongwa yenye urefu wa kilometa kumi kwa kiwango cha lami.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad