Mchana wa
saa tisa October 10 2014, Baba Levo ambae ni msanii wa bongofleva aliipigia simu
millardayo na kutoa taarifa za ajali aliyoipata saa saba mchana akitokea
Tabora kuelekea Mpanda ambako alikua anakwenda kwa ajili ya kutumbuiza.
Baba Levo
anasema alizitoa hizo taarifa saa tisa mchana sababu ndio aliweza kupata
angalau network ya mtandao wa simu kwani kwa saa mbili zilizopita alishindwa
kupiga simu baada ya kupata ajali porini kutokana na uzembe wa dereva wa
Coaster aliehama upande wake na kuhamia upande wa pili kukwepa barabara mbovu.
Kina Baba
Levo walikua kwenye Basi kubwa lililogongana uso kwa uso na Coaster hii ambapo
Baba Levo alikua amekaa pale mbele pembeni kabisa ya dereva kwenye kile
kigodoro ambapo msanii huyu ilibidi akae hapo sababu kiti chake kiliuzwa ticket
kwa watu wawili hivyo aliamua kuiachia siti yake kwa mama wa Kiarabu baada ya
kujikuta wote wamepangwa siti moja.
|
No comments:
Post a Comment