AJALI:-Kuanguka kwa Lori hili la Vinywaji…..ingetokea eneo lako ungefanyaje??...Tazama Picha 7 zake hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 11, 2014

AJALI:-Kuanguka kwa Lori hili la Vinywaji…..ingetokea eneo lako ungefanyaje??...Tazama Picha 7 zake hapa.

Kioo cha lori cha  mbele kikiwa kimepasuka. Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali baada ya  gari lililopata ajali.

 Watu watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea Jana October 09,2014, asubuhi maeneo ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu,  mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo  kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na  ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.

(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)


……………..Makreti ya soda yalivyoanguka………………

Pichani juu na chini ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo huku picha chini ni Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo husika.



Sehemu ya foleni iliyosababishwa na ajali ya gari hilo.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad