Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na Kamati ya Afya
ya Msingi mkoa wa Mwanza alisema ni wakati muafaka kwa jiji na halmashauri zake
kutoa elimu juu ya magonjwa hayo ili wananchi wajue dalili na namna ya
kujikinga na ugonjwa huo. Bw.Ndikilo alisema mkoa wake unapata wageni kutoka Uganda hususani wafanyabiashara wanaoleta bidhaa zao nchini kupitia Mutukula, na Watanzania wengi kwenda huko kwa sababu mbalimbali. KAMATI NDOGO YAUNDWA KAGERA. Katika kukabiliana na hilo, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera, umeunda kamati ndogo ya watu 19 kwa ajili ya kufuatilia magonjwa ya maburg na ebola. Dk. Rutachunzibwa Thomas, alisema kamati hiyo itakuwa inashughulikia masuala mbalimbali ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi. SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO). Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa huo umeongezeka kwa asilimia 70 na wagonjwa wapya wanaweza kuongezeka hadi kufikia 10,000 kwa wiki kwa kipindi cha miezi miwili. Taarifa hii imeandaliwa na Renatus Masuguliko, Sengerema, Pendo Paul, Mwanza Na Lilian Lugakingira, Bukoba/Nipashe.
Karibu
kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana
/Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, October 20, 2014
HOFU YA EBOLA SENGEREMA:-Ni baada ya mtu kufariki na kuhisiwa kuwa alikuwa na Ebola.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment