UHALIFU KAGERA:-Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo. ..Tazama Picha za tukio hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 11, 2014

UHALIFU KAGERA:-Kanisa la PAG Bukoba lavamiwa,wawili wakatwa mapanga,mmoja afa papo hapo. ..Tazama Picha za tukio hapa.


Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana October 10,2014, wamevamia Kanisa la PAG tawi la  Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa,hawakuiba chochote ikiwemo simu zao.


Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini na kwamba waliohusika na tukio hilo ni Wapinzani ya dini yao.



Mwandishi wa mtandao wa  www.harakatinews.com amefika katika eneo hilo na kushuhudia sehemu ya madhabahu ikiwa imetapakaa damu (tazama picha juu na chini ) na imeelezwa na mashuhuda kuwa damu husika ni wakati marehemu na mwenzake walipokuwa wakitaka kujinusuru kutoka kwa wakora hao.

Inaelezwa kuwa hadi wanatendewa kitendo husika walikuwemo peke yao  majira ya saa 8 usiku baada ya wenzao kuondoka katika baada ya  ibada usiku kumalizika saa 4 usiku hivyo wao waliamua kulala kanisani.



Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU  ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha dini huyo  mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.

Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadaye,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti Bukoba mjini,majeruhi  amelazwa hospital ya mkoa.

Viongozi wa makanisa ya PAG watatoa tamko rasmi saa 5 asubuhi hii .

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
Habari Na:-harakatinews.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad