ZIARA KASULU:-Hiki ndicho kilichotolewa wito kwa Wakimbizi Kambini Nyarugusu wakati Waziri Chikawe alipofanya ziara wilayani Kasulu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 14, 2014

ZIARA KASULU:-Hiki ndicho kilichotolewa wito kwa Wakimbizi Kambini Nyarugusu wakati Waziri Chikawe alipofanya ziara wilayani Kasulu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiwasalimia wacheza ngoma ya asili ya nchini Kongo iliyokuwa ikichezwa na wakimbizi wenye asili hiyo wakati alipokuwa anaingia katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma kwa ajili ya kuzungumza nao. 

 Waziri Chikawe alifanya mkutano na baadhi ya wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kambi hiyo inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. 

Katika hotuba yake Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi hao kupinga ndoa za utoto ambazo zinaendelezwa na baadhi ya familia za wakimbizi hao ambapo inawasababishia watoto hao wa kike kupata matatizo mbalimbali wakati wanapojifungua.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.Kushoto kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwasalimia watoto wa wakimbizi wakati Waziri huyo alipokuwa anatembelea baadhi ya familia za wakimbizi hao kwa lengo la kuwasalimia pamoja na kuangalia jinsi maisha yao wanavyoyaendesha kambini hapo. 

Waziri Chikawe alifanya mkutano na wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani na pia kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000... Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. 

Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad