SOKA TANZANIA:- Yanga SC imebeba Ngao ya Jamii kwa kuitungua Azam FC kwa mabao 3-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 14, 2014

SOKA TANZANIA:- Yanga SC imebeba Ngao ya Jamii kwa kuitungua Azam FC kwa mabao 3-0 .


Kocha Marcio Maximo akimpongeza Genilson Santana 'Jaja' baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC mechi ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Septemba 14,2014. 

 Jaja alifunga  mabao yake katika dakika ya 56 kabla ya kupachika la pili katika dakika ya 65 huku Balo lingine lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 88 baada ya kipa Mwadini Ally kujichanganya na mfungaji akautupia nyavuni kwa ulaini kabisa.

Pamoja na kuifunga Azam FC, Yanga imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania Bara kuifunga Azam FC ambayo ilimaliza mechi 26 bila kufungwa hata moja.

Azam FC ilicheza vizuri na kutawala kipindi cha kwanza, lakini mambo yakabadilika katika kipindi cha pili.



LIGI KUU SOKA VODACOM TANZANIA BARA 2014/2015.

Mechi za Ufunguzi-Jumamosi Septemba 20,2014.

Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]

Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]

Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]

Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]

Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]

Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]

Septemba 21,2014.

Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

MECHI ZA MOTO-DABI YA KARIAKOO.

12-10-14 Yanga v Simba [Uwanja wa Taifa, Dar]
 
08-02-15 Simba v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar]

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad