UHALIFU:- Afisa Usalama Feki na Silaha zakamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 03, 2014

UHALIFU:- Afisa Usalama Feki na Silaha zakamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania.

Baadhi ya silaha zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kamanda Suleiman Kova akionyesha  silaha zilizokamatwa kwa wanahabari (hawapo pichani).
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kamanda Kova.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam,  kwa tuhuma za kujifanya  mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa .

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa.

Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata  bastola nne na shot-gun moja wiki hii.

Na Gabriel Ng’osha/GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad