|
Mtu mmoja ambaye ni dereva
aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki
dunia katika ajali mbaya huku mtoto wake
akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane
hapa jijini Mbeya usiku wa kuamkia jana Septemba 01,2014 majira ya saa saba za usiku.
Dereva huyo aliyefariki dunia
amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba alifariki dunia baada ya gari hilo
kuacha njia na kupinduka katika maeneo hayo ya Nane Nane achali iliyopelekea
pia kujeruhiwa kwa mtoto wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba
mwenye miaka 7 na mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika
hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Mpaka sasa chanzo cha ajali
hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini,
lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya
moto kwa kuzingata sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali
zinazoweza kuepukika.
|
No comments:
Post a Comment