Katika
mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka,
ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo
hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata
kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii
ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu
kutumia pesa zao.
Duka
lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri
watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika
historia ya nchi hii.
Kulingana na
taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika
kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola
bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la
Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa
sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya
kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo
tofauti wa Picha'
''Watu
wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki
wa duka hili Tina Liu.
"maharusi
huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''
|
No comments:
Post a Comment