UCHAGUZI BENACO:-Huyu ndiye Kiongozi wa Msikiti wa Benaco akichaguliwa kwa kupata kura 88. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 11, 2014

UCHAGUZI BENACO:-Huyu ndiye Kiongozi wa Msikiti wa Benaco akichaguliwa kwa kupata kura 88.

Waumini na viongozi wa taasisi mbalimbali za dini ya kiislamu wilayani Ngara mkoani Kagera,wametakiwa kuishi bila kubaguana kutokana na tofauti za itikadi zao kimadhehebu  bali washirikiane kwa  kudumisha umoja wao na kuelimishana ili kupata  maendeleo.

Mjumbe wa baraza kuu la waislamu BAKWATA wilayani Ngara mkoani Kagera Bw Hussen Msema amesema hayo Septemba 07,2014,katika msikiti wa mtaa wa Benaco kata ya Kasulo wakati akisimamia uchaguzi wa imamu wa kuongoza msikiti wa mtaa huo.

Bw Msema amedai kuwa    kuongoza watu kunahitaji hekima na busara katika kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kujihadhari na matumizi ya ulimi ambao  unaweza  kusababisha kuvunjika kwa  Amani katika eneo husika.

 Mwenyekiti wa BAKWATA  wilayani Ngara, Sheikh Rajabu Msabaha amemtangaza Bw Adamu Juma Mrangi kuwa Imamu wa Msikiti wa Benaco baada ya kupata kura 88 dhidi ya mpinzani wake Rajabu Mwarobaini aliyepata kura 16
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad