HUU KWELI MCHARUKO:-Wazimu wake unapompanda Balotelli…………’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 11, 2014

HUU KWELI MCHARUKO:-Wazimu wake unapompanda Balotelli…………’’


Mshambuliaji Mario Balotelli jana aliteremsha bukta yake namna hii mazoezini Melwood akiwa na timu yake Liverpool. Huu ni mfululizo wa vituko vya mshambuliaji huyo.


Pamoja na vituko vyake ,Liverpool ilifanikiwa kuingiza pauni 50,000 kupitia mauzo ya jezi za Mario Balotelli, siku ya kwanza tu baada ya kumsajili.

Balotelli ,24, amejiunga na Liverpool akitokea AC Milan kwa kitita cha pauni milioni 16.

Mashabiki wa Liverpool wakampokea wakionyesha wanamkubali wakinunua jezi zake kwa wingi na kuiingizia klabu yao pauni 50,000 ambayo ni rekodi kwa mauzo ya siku moja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amethibitisha hilo na kuonyesha nguvu ya mashabiki wa klabu hiyo kongwe yenye mashabiki wenye moyo wa chuma.

Mtaliano huyo alifunga mabao 20 katika mechi 54 akiwa na Manchester City katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 alipoondoka kwenda AC Milan.
 

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad