Matumizi ya
dawa za kienyeji kwa ajili ya kuongeza uchungu na kujifungua mapema, imeelezwa
kuchangia zaidi vifo kwa wajawazito.
Mganga Mkuu
wa Mkoa Kigoma, Dk Leonald Subi alisema hayo mjini Kigoma kwenye kikao cha
wadau wa afya kilichokuwa na lengo la kufanya tathmini na kuona hatua za kuchukua kukabiliana na vifo vya
wajawazito na watoto wakati wa kujifungua mkoani Kigoma.
Katika Kikao hicho kilichoitishwa
na shirika la Wolrd Lung Foundation, Dk Subi alisema kuwa licha ya jitihada
mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine,
kukabiliana na hali hiyo, bado wajawazito wanajifungulia majumbani na kutumia
dawa hizo hatarishi kwa maisha yao.
Alisema
kumekuwa na upungufu wa vifo vya wajawazito na ongezeko la vifo vya watoto ambapo vifo
vya wajawazito vimepungua kutoka vifo 74 mwaka 2009 hadi kufikia 49 kwa mwaka
jana ( 2013) huku vifo vya watoto wachanga vikiongezeka kutoka 720 mwaka 2009 na
kufikia 840 mwaka jana 2013.
Mkurugenzi
wa Miradi wa World Lung Foundation, Dk Nguke Mwakatundu alisema shirika lake
linaboresha huduma za mama na mtoto mkoani humo, lakini changamoto ya vifo vya
wajawazito ni kubwa, kutokana na kujifungulia majumbani.
|
No comments:
Post a Comment