|
Mwakilishi wa Timu ya Simba akipokea kutoka
kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto) jezi
zitakazotumiwa na timu hiyo katika msimu huu mpya wa 2014/2015 utakaoanza Septemba 20,2014.
Pili toka kusho ni Afisa mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga na
kulia ni Mjumbe wa TFF na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange.
Vodacom
imekabidhi vifaa kwa timu zote 14 zitakazoshiriki ligi kuu vikiwa na thamani ya
zaidi ya shilingi Milioni 430.
|
|
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania
Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Silas Mwakibinga na kulia ni
Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakifurahia jambo pamoja na Afisa habari wa Yanga
Baraka Kizuguto wane toka kushoto wakati wa hafla ya Vodacom kukabidhi vifaa
kwa timu 14 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.
|
|
Mwakilishi wa timuu ya Mbeya City akipokea
kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto)
jezi zitakazotumiwa na timu hiyo katika msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu ya
Vodacom.
Wa pili toka kusho ni Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas
Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange.
|
|
Kutoka kushoto: Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas
Mwakibinga,Mwakilishi wa timu ya Kagera Sugar na Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange
wakionesha jezi ilziokabidhiwa timu ya Kagera kwa na kampuni ya Vodacom kwa
ajili ya msimu wa 2014/2015. Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14
zinazoshiriki ligi hiyo.
|
|
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania
Salum Mwalim(kushoto) akimkabidhi jezi Mwakilishi wa JKT Ruvu akishuhudiwa na
Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga(katikati) wakati wa hafla
ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom.Vifaa hivyo zimetolewa na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
|
|
AfisaMendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas
Mwakibinga(katikati)akipokea vifaa vipya toka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Tanzania Salum Mwalim, vitakavyotumiwa na waamuzi katika mechi
mbalimbali za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazoanza hivi karibuni.
Jumla ya zaidi ya shilingi Milioni 430 zimetumika katika kununua vifaa kwa timu
14 zitakazoshirikii Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015 pamoja na vifaa vya waamuzi.
|
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Timu zote 14
zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom,
Mlimani City, Dar es Salaam.
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam FC
wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam.
Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya
Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20,2014.
Mechi
nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha
Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha
Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa
Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji
hilo Septemba 21,2014 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki
hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.
No comments:
Post a Comment