KASI YA AJALI TANZANIA:-Hii ndio idadi ya Vifo vingi zaidi kuliko Ajali zilizotokea nyuma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 11, 2014

KASI YA AJALI TANZANIA:-Hii ndio idadi ya Vifo vingi zaidi kuliko Ajali zilizotokea nyuma.


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania ,Bw. Mohamed Mpinga, amesema ajali zilizotokea katika kipindi cha miezi ya Juni, Julai na Agosti  mwaka  huu wa 2014, zimesababisha vifo vingi zaidi  kuliko ajali zilizotokea kipindi cha  nyuma.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Septemba 10,2014 jijini Dar es Salam,Kamanda Mpinga alisema kuwa  jumla ya vifo vilivyotokea kipindi cha miezi hiyo pekee ni asilimia 70, huku akitaja watu waliokufa katika  Juni kuwa ni 320, Julai 388 na Agosti ni 390.

Alisema kwa Juni ajali zilizotokea ni 1157, Julai 1035 na Agosti ni 1146.

Kwa upande wa ajali zilizotokea Mkoani Mara, Morogoro na sehemu nyingine wiki hii, Mpinga alisema wamebaini chanzo kikibwa cha ajali hizo ni uzembe wa madereva.

Alisema bado wanafanya uchunguzi kwa magari hayo na madereva ili kubaini kama yana ubora wa usafirishaji na endapo watabaini mapungufu watawachukulia hatua.

Aidha,  Jeshi hilo limepokea vifaa vya usalama barabarani kutoka kwa Kampuni ya Scania kwa ajili ya kusaidia shughuli za usalama.
 UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad