Baadhi ya
watu wameku wakituma picha za simu zao zilizojipinda.
Russell
Holly, anayefanyia kazi mtandao wa habari wa geek.com,ni mmoja wa wale
walioripoti kuwa simu yake imejipinda.
Watumiaji wa
mtandao wa kijamii wa Twitter, wametu moani yao kuhusu habari za simu hiyo
kujipinda.
BBC
ilijaribu kuwasiliana na Apple kuhusu ripoti hizo lakini haijasema chochote mpaka
sasa.
Mmoja wa
wataalamu wa maswala ya kiteknolojia, anasema kuwa kampuni ya Apple inapaswa
kuchunguza malalamiko hayo na hata kutoa taarifa rasmi haraka iwezekanavyo.
Jasdeep
Badyal anasema kuwa Apple inapaswa kujibu madai hayo na kisha ikiwa ni kweli,
basi inapaswa kuchukua hatua ya kuwapa simu mpya watu walioripoti kuwa simu zao
zimejipinda.
Aliongeza
kuwa hata kama kulikuwa na simu kdhaa tu zenye tatizo hilo, kampuni hiyo
inapaswa kutoa taarifa na kueleza kilichofanyika.
|
No comments:
Post a Comment