HomeMATUKIODEMOKRASIA:-Yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera September 25,2014.
DEMOKRASIA:-Yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera September 25,2014.
Wagombea wenye sifa wakijinadi mbele ya
Wananchama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa
Halmashauri wa Wilaya ya Ngara,walishiriki uchaguzi mkuu kwa kuchagua Viongozi
wengine wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka 3 -NDCW-SACCOS,katika mkutano mkuu maalumu uliofanyika Septemba 25,2014 katika Ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya mjini Ngara.
Mwenyekiti aliyemaliza
muda wake Bw.Benjamin Yusuf (kushoto) katika taarifa yake kwa Wanachama ,amebainisha kuwa chini
ya uongozi wake Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa
Halmashauri ya Wailaya ya Ngara-NDCW-SACCOS ilikuwa na Wanachama 917 hadi
akitoa taarifa yake NDCW-SACCOS ina Wanachama 1030.(Ongezeko ni Wanachama 113).
Pia alisema
mtaji wa Chama na Bima ulikuwa Zaidi ya Shilingi Bilioni 3.4,ambapo kwa Kipindi
hiki umeongezeka hadi kufikia Bilioni 4.1 sawa na Ongezeko la Shilingi Milioni
700.
Pamoja na
mafanikio ,Chama kimekuwa kikipambana na changamoto mbalimbali ambazo ni :-
·Fedha inayotoka hazina kupitia kwa
Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngara,kuchelewa,sehemu ya fedha hiyo imeishalipwa. ·Baadhi ya wanachama kuomba kuchukua
akiba badala ya kukopa. ·Baadhi ya wanachama kutokuwa
waaminifu,kwani tunapokwenda benki tunakuta fedha zao zimeshakatwa na
wanaowadai kupitia Hazina.
·Kutokana na changamoto hizo
,mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw.Benjamini Yusuf alisema zimekuwa
zikisababisha Huduma yetu nzuri kutokamilika kwa wakati.Aidha aliwaomba
wanachama wenye tabia hiyo wabadilike.
Msimamizi
Mkuu wa Uchaguzi huo , Afisa Ushirika wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Ganashi
Levinus Kulwa alisema uchaguzi huo umefanyika kufuatia agizo la Serikali chini
ya Sheria mpya ya Vyama vya Ushirika Tanzania namba 6 ya mwaka 2013 ambayo
imeanza kufanya kazi mwaka huu 2014.
Ni Baadhi ya
Wanachama hai 294 wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa
Halmashauri wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera NDCW-SACCOSwakifatilia kile kilichokuwa kikiendelea
katika Mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi wa Wajumbe wa Bodi kwenye ukumbi wa
Halmashauri Mjini Ngara September 25,2014.
Katika
uchaguzi,Msimamizi Bw.Ganashi aliwatangaza Wajumbe 9 wa Bodi waliochaguliwa
kuwa ni:-
Bw.JacksoniKanani –kura 50.
Dr.David
Mapunda – kura 46.
Bw.Alphonce
Wisize – kura 44.
Bw.Josias
Kimuga – kura 30.
Bw.Benjamin
Yusuf – kura 26.
Bw.Theonest
Thadeo – kura 17.
Bi.Jeniva
Nyamkara – kura 13.
Bw.Medani
Bagege –kura 11.
Bw.Emanuel
Buberwa –kura 7.
Jumla ya Wapiga kura walikuwa 272 ambapo kura 2 ziliharibika.
Upande wa
Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa ni:-Bw.Joasia
Kimuga pichani kushoto,kwa –kura 99 akiwashinda
Bi.Jeniva Nyamkara aliyepata kura 82 .
Na Bw.Medani Jekamaya
kura 52 ambapo jumla ya kura zilikuwa ni 234 na iliyoharibika ni Moja.
KATIKA Nafasi
ya Mwenyekiti wa NDCW-SACCOS iliyokuwa na Ushindani mkubwa,alichaguliwa
Mwl.Jackson
Kanani- kura 72 akiwashinda washindani
wake,
Dr.David
Mapunda – kura 63.
Bw.Alphonce
Wisize – kura 48.
Bw.Benjamini
Yusuf – kura 39 (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake)
Bw.Theonest Thadeo – kura 15.
Katika
nafasi hii jumla ya kura 257 zilipigwa.
Ni Baadhi ya
Wanachama hai 294 wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa
Halmashauri wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera NDCW-SACCOSwakifatilia kile kilichokuwa kikiendelea
katika Mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi wa Wajumbe wa Bodi kwenye ukumbi wa
Halmashauri Mjini Ngara September 25,2014.
Wajumbe wa
Kamati ya Mikopo waliochaguliwa katika Uchaguzi huo ni :-
Dr.David
Mapunda – kura 67.
Alphonce
Wisize – kura 50.
Bi.Jeniva
Nyamkara – kura 34.
Na Wajumbe
wa Kamati ya Usimamizi waliochaguliwa ni:-
Bw.Seledi
Mudiguza – kura 107.
Bi.Gradis
Samugabo – kura 26.
Bw.Christopha
Nzoya - kura 24.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment