Watu
watano wakazi wa kijiji cha Litapwasi wilaya ya Songea wanashikiliwa na
polisi Mkoani Ruvuma kwa mahojiano zaidi kufuatia watu 246 kulazwa katika
hospitali ya Misheni Peramiho na kituo maalumu kilichoandaliwa katika zahanati
ya kijiji cha Ligweneni baada ya kunywa togwa ya kienyeji inayodhaniwa kuwa na
sumu.
Kamanda wa
polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea jana
mchana katika kijiji cha Litapwasi nyumbani kwa Ines Nungu (47)
ambako kulikuwa na sherehe ya ubarikio wa kipaimara cha watoto wake 2.
Kamanda
Msikhela amesema kuwa katika sherehe hiyo kulikuwa kumeandaliwa vyakula
mbalimbali, vinywaji ikiwemo togwa iliyotengenezwa kienyeji ambayo imeonekana
kuwa watu wengi ambao waliohudhuria kwenye sherehe hivyo walikunywa kwa wingi.
Alisema
katika sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali
za vijiji vya Liagweni,Sinai,Likulufusi na Songea Mjini kulikuwa na kinywaji
cha togwa ambacho walikuwa wakijihudumia wao wenyewe pale wanapohitaji.
Alifafanua
kuwa katika sherehe hiyo kulikuwa na vyakula vingi pamoja na togwa lakini
inaonekana kuwa watu waliokula vyakula bila ya kunywa togwa hawakuathirika na
hali zao zinaendelea vizuri.
Alisema
baada ya muda mfupi watu waliokunywa na kutawanyika kurudi majumbani kwao
ambako walianza kuharisha na kutapika.
|
No comments:
Post a Comment