Alfred
Tibaigana alipokuwa kazini siku chache kabla ya kustaafu.
Katika
mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba,mkoani Kagera,
Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa
kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama
vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo
yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu.
“Pengine
hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na
wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama
kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.
“Kikubwa ni
kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao,
vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa
maandamano yao,” alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai
maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.
“Nilikuwa
nawaita viongozi nakaa nao tunakubaliana. Hata kama ningeambiwa na kiongozi
gani nisitoe kibali, kama hakuna sababu za kweli, nilikataa kwa kuwa kisheria
mimi ndiye nawajibika kama vyama vikishtaki. Ili uzuie maandamano unapaswa kuwa
na sababu za msingi ambazo ukiwaeleza waandamanaji wanakuelewa.”
Tibaigana
anakumbuka jinsi CUF kilivyoandaa maandamano makubwa kushinikiza kuundwa kwa
serikali ya mseto visiwani Zanzibar baada ya kutoridhishwa na matokeo ya
Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, lakini anasema kutokana na msimamo wake, haikuwa
vigumu kwake kuruhusu jambo hilo.
|
No comments:
Post a Comment