AFYA YAKO:-UTI kwa Wanaume na Wanawake na NGONO. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 17, 2014

AFYA YAKO:-UTI kwa Wanaume na Wanawake na NGONO.

Huu ni ugonjwa wa Watanzania wengi miongoni mwetu, kupima Afya mpaka aumwe azidiwe, lakini angepima na kujua afya yake mapema asingefikia hatua ya kuugua na hata kufikia kulazwa. Anaongeza gharama nyingi za matibabu na pia kukwamisha kazi. Jali Afya Yako. MUUNGWA NI VITENDO. 

 Sasa Ugonjwa wa UTI - kirefu chake ni Urinary tract infection, hawa ni bakteria ambao kila mmoja wetu anao sema  wanapatikana wengi zaidi kwenye sehemu ya haja kubwa. 

Bakteria hawa kama wakikutana na sehemu yako ya kizazi yaani uume {kwa Mwanaume} au uke {kwa Mwanamke} wanaingia na kusafiri kwenye njia ya mkojo yaani urethra , kama ukichelewa matibabu huenda mpaka wakafika kwenye kibofu cha mkojo, ambacho wadudu hawa ndo hua wanakishambulia kwa kubomoa kuta za kibofu hivyo kusababisha mabadiriko ya mwili wako kama vile:-

  • Kukojoa mara kwa mara
 
  • Kusikia maumivu wakati wa kukojoa
 
  • Muda mwingine hata kuwashwa kwa ndani
Inashauriwa ukishasikia dalili hizi uwahi mara moja hospitali ili waweze kukutibia. 

Nini kitatokea kama usipoenda Hospitali.

  • Wanaweza kusababisha ukosefu wa kuweza kuzaa kwa mwanamke au mwanaume, hii ni kutokana na kwamba, jinsi wanavyozidi kua wengi ndivyo wanavyoshambulia zaidi viungo vya uzazi.
 
  • Kidney failure. wanaweza wakapanda kwenye mfumo wa mkojo na kwenda mpaka kwenye kidney ambapo watalishambulia sana na kulifanya lishindwe kufanya kazi linavyotakiwa.
Wahi ukapime sasa.

JINSI GANI UNAWEZA PATA UTI.

Kwa wanaume inakua ni ngumu kidogo kuupata na hata wakipata inakua ngumu kuona dalili zake mapema.ila kwa mwanamke ni rahisi kupata UTI na kwa haraka dalili zitajionyesha.

Wanawake.

kutokana na mfumo wa viungo vyao  vya uzazi vilivyokaa, kibofu kipo karibu sana na sehemu ya kukojolea, hivyo mrija wake wa urethra ni mfupi sana kutoka sehemu ya kutolea mkojo ambayo ipo juu kidogo na sehemu ya kufanyia mapenzi {ukipaangalia kwa haraka unaweza usipaone, ni kishimo kidogo sana}, na kibofu chao kimekaa kwa juu kidogo chini ya uzio wa tumbo hivyo kufanya njia yake kua fupi sana.
Kwa wanawake kupata UTI ni rahisi kutokana na hizi sababu, zifuatazo ni njia ambazo mwanamke ataweza pata UTI.

  • Vyoo vichafu na vile vya Public   
          Kwa mwanamke kutumia vyoo vichafu hii ni mbaya sana kwake au kwenda mara kwa mara kwenye vyoo vya public kama vile vilivyo kwenye stand za bus, sio nzuri kwasababu watu wakila aina wanaenda pale, na jinsi wanavyokojoa hua wanachuchumaa hivyo kufanya iwe rahisi kwa majimaji kurukia kwenye uke wao na kueneza vijidudu hivi.  

Kuepukana na hii, inabidi mwanamke anapoenda kukojoa asichuchumae kabisa chini bali awe kama amesimama na ainue skirt yake vizuri au avue suruali yake vizuri kisha akojoe, na akimaliza ahakikishe anajifuta vizuri uke wake ili kuwa msafi.

  • Kuoga mara kwa mara
     Hii nayo haishauriwi sana, jinsi unavyojiweka katika hali ya kulowana lowana huko maeneo ya ukeni unaruhusu uwezekano wa vijidudu kusafiri kutoka kwenye sehemu yako ya haja kubwa na kuingia kwenye uke wako. 

Kuzuia hii, inabidi pindi unapooga wakati wa kujisafisha uke wako usimwage maji kutokea sehemu ya nyuma bali yamwagie maji kutokea kwa mbele kwenye mashavu ya uke na uyapeleke maji kwa nyuma, hii njia uitumie pia kipindi unaponawa labda ukitoka kukojoa au hata ukiwa unajishafisha, maji inabidi uyamimine kutokea kwa mbele yaende nyuma {sehemu ya haja kubwa}

  •  Chupi chafu
     kama wewe ni mwanamke na hua hufui nguo zako za ndani, inabidi uanze sasa kufua nguo zako ili kuukinga uke wako na magonjwa mbalimbali ukiachilia UTI, na kama una bwana wako na anakuvuaga nguo ukiwa na chupi chafu, basi hana akili na hakujali. inabidi uwe msafi ukeni ili kujilinda.

Mwanaume.

KAMA nilivyosema, mwanaume kupata UTI ni vigumu, kwakua yeye akienda chooni hachuchumai kama mwanamke na pia njia ya mojo yaani urethra yake ni ndefu sana, hivyo hata kama vijidudu vikiingia kwenye uume vitapata shida sana na vitachukua mda mrefu mpaka vifike kwenye kibofu kutokana na kwamba kipindi anapokojoa hua anaondoa vijidudu hivyo ingawa sio vyote lakini asilimia kubwa vinatoka.

Njia ambayo anaweza kupata UTI

  • Uchafu, {boxer chafu}
     Uchafu unaweza kukusababishia kupata UTI, kwakua unaweza ukawa umewabeba vijidudu kwa mda kwenye boxer yako na kila siku unaiweka kwenye uume wako hivyo vijidudu vitaingia na kuingia mpaka vitakuletea matatizo. hivyo inabidi muwe wasafi pia.

  • Ngono.

Kuingiliana kimwili ni njia kubwa ya kueneza magonjwa na bakteria wa kila aina, kwa kua mnakua mnashirikiana na kupeana majimaji yanayotoka katika kila mwili wa mwenzako, kipindi mkutanapo kimwili, kwa mfano mwanamke hana UTI na mwanaume anayo, wakati anakutia wewe mwanamke uume wake unakua upo ndani ya uke wako, na kwakua uume hua unatoa majimaji yanayoitwa semen, haya maji maji hua yanabeba hivyo vijidudu na kuvihamishia kwenye uke wako, na wakishaingia ukeni basi, umeshapata UTI.

Vivyo hivyo kwa mwanaume, hii ndo njia kubwa pekee kwa mwanaume kupata UTI, kwakua anakua anaingiza uume wake kwa mda mrefu kwenye ulimwengu wa majimaji ya ukeni na hivyo inakua rahisi kwa vijidudu kuhamia kwenye uume wake kupitia majimaji hayo. 

Pia kupitia NGONO, uzalishaji wa hawa vijidudu unakua ni mkubwa kwa sababu hii: -
  •  Mwanaume anapokojoa shahawa zake, hizo shahawa ni kama chakula kwa hawa vijidudu, hivyo kuongeza kasi ya hawa vijidudu kuzaliana kwa kasi sana na kukusababishia maumivu kwa pande zote mbili {mwanaume na mwanamke}, na ndio maana ukiwa unatumia dawa za  kutibu UTI madaktari hua wanashauri usifanye mapenzi mpaka utakapo maliza kutumia dawa, hii ni kutokana na kwamba mbegu za mwanaume zinachangia uzalishaji wa hawa wadudu kwa uwingi na kasi zaidi.

USHAURI:-KWA KUJUA HAYO, WOTE MJIKINGE NA MJILINDE, TUMIA CONDOM KAMA UNAONA UMWAMINI MWEZA WAKO, NA KAMA NI MWANAUME HATAKI KUTUMIA CONDOM LABDA KWASABABU HUA HASIKII UTAMU, BASI WEWE KAMA MWANAMKE NUNU CONDOM ZA KIKE NA UIVAE NA UFANYE TENDO LA NGONO.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad