PICHA / UHALIFU TANZANIA:- Bomu limejeruhi Askari Polisi Watatu wilayani Songea mkoani Ruvuma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 17, 2014

PICHA / UHALIFU TANZANIA:- Bomu limejeruhi Askari Polisi Watatu wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa Kazini.

 Wakazi wa mji wa Songea wamekumbwa na taharuki baada ya bomu linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji kurushwa na watu wasiojulikana katika kata ya Misufini mkabala na kata ya Matarawe  wilayani Songea mkoani Ruvuma na kuwajeruhi askari polisi wawili waliokuwa doria maeneo hayo na kutoa kishindo kikubwa.

Tukio hilo limetokea  September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma  ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari  hao watatu waliokuwa doria.

Askari hao waliojeruhiwa ni  WP. 10399 PC Felista Makala  aliyejeruhiwa mguu wa kulia  kwenye unyayo na pajani  ,G. 7351 PC Ramadhan Ally aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na  G. 5515 PC John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

Aliyelala kitandani ni WP Felista Makala ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma.

Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi ambapo Kutokana na kishindo cha bomu hilo vioo vya nyumba za jirani na lilikorushwa bomu vimepasuka  huku polisi wakiweka vizuizi eneo la tukio.


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu akiwa ameongozana na kamati yake ya ulinzi na usala  amewatembelea majeruhi wa tukio hilo katika hospitali ya mkoa wa ruvuma na kusema hilo ni tukio la kiharifu na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

Amesema  amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
 Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo, ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

Aidha  kufutia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi  wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria na kwamba Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini DCP Isaya Munguru atatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na tukio hilo atakapowasili mkoani Ruvuma
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad