UTAMADUNI WETU:- Tazama Picha wakati Rais Kikwete akitawazwa kuwa Chifu msaidizi wa Waluguru na chifu kingalu huko kinole, morogoro, apewa jina la Chidukila. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 23, 2014

UTAMADUNI WETU:- Tazama Picha wakati Rais Kikwete akitawazwa kuwa Chifu msaidizi wa Waluguru na chifu kingalu huko kinole, morogoro, apewa jina la Chidukila.

Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila (Rais Jakaya Mrisho Kikwete) akifurahia Pama lake wakati alipotawazwa na CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.

   Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.


Umati wa wananchi ukimsikiliza Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila wakati wa sherehe hizo.


Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akiongea na wananchi wakati wa sherehe hizo.

 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika  mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimuonesha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete namna ya kuweka kifimbo maalumu begani wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo.

Mke wa Chifu Kingalu akimkabidhi Mama Salma Kikwete shuka katika sherehe hizo.

Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia wakati wa sherehe hizo.

Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia kifimbo maalumu alichokabidhiwa wakati wa sherehe hizo.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14 akibadilishana mawazo na Rais Kikwete wakiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera na kushoto ni msaidizi wa Chifu Kingalu.

Mama Salma Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, akisisitiza umuhimu wa kinamama kujiunga na SACCOS pamoja na kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa wakati muafaka.

Rais Kikwete akiwaaga wananchi wa Kinole baada ya sherehe hizo.

PICHA NA IKULU
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad