SOKA LA MAVETERANI:- Mkongwe Luis Figo aongoza Real Madrid kuwapa raha Mashabiki wao kwa kuifunga 3-1 Tanzania mbele ya Rais Kikwete. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 23, 2014

SOKA LA MAVETERANI:- Mkongwe Luis Figo aongoza Real Madrid kuwapa raha Mashabiki wao kwa kuifunga 3-1 Tanzania mbele ya Rais Kikwete.



Reuben De La Red kushoto amefunga mabao matatu peke yake wakati Real Madrid Maveterani ikishinda 3-1 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 23,2014 dhidi ya Tanzania Eleven.

De la Red alimfunga bao moja Mohamed Mwameja kipindi cha kwanza na kipindi cha pil akamtungua mara mbili Peter Manyika , wakati bao pekee la Tanzania Eleven Stars, Real Madrid walijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira De La Red baada ya mechi kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi huo.

Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, De La Red akimalizia pasi ya Luis Figo.



.........Luis Figo akimtoka Athumani China............
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Agosti 23,2014 na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete.


Beki wa Tanzania, Nsajigwa Shadrack kushoto akimtoka Fernando Sanz wa Real Madird. 
  

Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa. 

Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao kwa pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari.

Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje.

De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven. 

Wachezaji wa timu zote mbili wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye. 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad