Ukatili dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi (Albino) umejitokeza tena mkoani
Tabora ambapo mtoto Pendo Sengerema (14) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya
msingi Nundu, amekatwa mkoni wake wa kulia na wahalifu kukimbia nao
kusikojulikana na aliyeshiriki uharifu huo akihaidiwa kulipwa laki tisa huko
katika kijiji cha Usinge wilayani Kaliua.
Akiongea kwa tabu alipolazwa katika hospitali ya wilaya ya Urambo,
majeruhi Pendo Sengerema amesema kuwa, aliyemkata mkono alimfahamu maana
ni jirani anayesadikiwa kuwa, ni mganga wa kienyeji, ambapo kaimu mganga wa
hospitali hiyo, Dr. James Kang’oma, akidai kuwa walijitahidi kuokoa
maisha yake kutokanana na kuvuja damu nyingi.
Mratibu wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi wilaya za Urambo na Kaliua Bw
Focus Mgesera, amesema kuwa pamoja na mtoto huyo kulazwa katika hospitali hiyo
bado kuna hali ya hatali kwake kwani kwa namna moja ama nyingine anaweza kuuawa
kutokana na kuwafahamu waliomjeruhi, hivyo anahitaji ulinzi.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Under the same sun, Bi Vicky Ntetemya
aliyefika hospitalini hapo kumwona mtoto huyo amesema kuwa, serikali iwe makini
na jamii ya wenye ulemavu wa ngozi kutokana na masuala ya wagombea nafasi za
uongozi kujishirikisha ma mambo ya waganga wa kienyeji.
Chama cha Walemavu wa ngozi nchini kimeraani tukio hilo kikitaka serikali
kuongeza ulinzi kwa jamii hiyo ambapo akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa
Polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda akidhibitisha kutokeaa tukio hilo.
|
No comments:
Post a Comment