Mkurugenzi
wa Mafunzo na Uchaguzi wa CHADEMA, Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani). (Picha na Maktaba).
|
Alisema kuwa
mkutano mkuu wa mkoa ulikuwa na mamlaka yote ya kuamua kuchagua uongozi kwa
ajili ya kuendesha chama kipindi ambapo kuna baadhi ya viongozi wametoka.
Aliyechaguliwa
kuwa Katibu wa Mkoa wa Kigoma, alimtaja kuwa ni Shabaan Madebe wakati nafasi ya Mratibu wa
Baraza la Wanawake wa mkoa huo (BAWACHA), ilichukuliwa na Vestina Luhihi.
Omary Gindi
alichaguliwa kuwa Mratibu wa Baraza la Vijana mkoa wa Kigoma wakati Jeremia
Misigara alichaguliwa kuwa Mratibu wa Baraza la Wazee.
“Tumefanya
pia uchaguzi wa viongozi wa Jimbo la Kigoma mjini ambako Mwenyekiti
aliyechaguliwa ni Khalfani Bona na Katibu wake ni Frank Luhasha.
“Katibu
Mwenezi ni Idd Ngesha na Mratibu wa Wazee ni Yassin Mapigo wakati Amfua
Athumani ni Mratibu wa BAVICHA,” alisema Kigaila.
Kwa mujibu
wa Kigaila, viongozi hao waliochaguliwa wanatakiwa kuanza kazi mara moja na
jukumu lao kuu ni kukifanya Chadema Mkoa wa Kigoma kizidi kusonga mbele.
“Tumeshawahoji
hawa makamanda mmoja mmoja kama kazi hiyo tuliyowapa ya uongozi wataifanya kwa
moyo wao wa kujitolea bila ya malalamiko nao wametuahidi hawatatuangusha.
“Pia nimewaambia
wafanye kazi kwa moyo wa kujitolea na siyo kuwa ndani ya chama nusu nusu yaani
mguu mmoja ndani na mwingine nje,” alisema Kigaila.
Akizungumzia
chama kipya cha ACT, alisema hakijaleta madhara mkoani Kigoma dhidi ya Chadema.
Mwenyekiti
mpya wa Mkoa Kigoma, Ally Kisala, alisema pamoja na mkoa huo kuwa na changamoto
nyingi za siasa, atashirikiana na viongozi wenzake kukiimarisha chama chao.
Julai 18,2014
waliokuwa viongozi wa CHADEMA, Mkoa wa Kigoma ambao ni Mwenyekiti Jafari
Ramadhani Kasisiko,Msafiri Husein Wamalwa,Katibu, na Malunga Masoud Simba,
Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema, BAWACHA, walitangaza kujiuzulu nyadhifa
na uanachama wa CHADEMA.
Walisema
walichukua hatua hiyo baada ya kuona kuwa CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama
cha kidemokrasia na kuwa chama cha kibabe.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment