........Dk. Willbrod Slaa kushoto na John Mnyika kulia...... |
Madiwani
walioasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamerejea na kudai
walirubuniwa na makada watano wa CCM kuhama kwenye chama hicho ili wawatumie
kuwaua, Dk. Willbrod Slaa na John Mnyika.
Madiwani hao
ni Sebastian Mzuka wa kata ya Ngokolo na Zacharia Martin wa kata ya Masekelo
wote kutoka Shinganya mjini ambao wamewataja makada hao kuwa ni Naibu wa Waziri
wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Wengine ni
Naibu waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele ambaye pia ni Mbunge wa
Shinyanga mjini, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC, chama tawala, Nape Nnauye,
na Habibu Mchange (aliyefukuzwa Chadema).
Wakizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama hicho,
madiwani hao walisema kuwa, mauaji hayo yalipangwa kutekelezwa kwa kiasi cha
Sh. milioni 180.
Diwani Mzuka
alisema wamefika kwenye ofisi hizo ili kueleza kinachoendelea kudhoofisha chama
na kuomba toba baada ya kuhama.
Alisema mara
baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuvuliwa madaraka Chadema,
Mchange alipewa kazi (dili) na CCM kutafuta viongozi na madiwani wa Chadema
lengo likiwa ni kukidhoofisha.
Alisema
Mchange aliwafuata Shinyanga kuzungumza nao kuhusu suala hilo.
Alisema
Januari 27, mwaka huu alipewa kazi ya kulipua helkopta iliyokuwa ikitumiwa na
Katibu Mkuu Chadema, Dk. Slaa, Mbunge wa Ubungo, Mnyika na Mwenyekiti wa kanda
ya Mashariki katika ziara ya Kanda ya Ziwa.
“Aliniambia
kuwa Masele ana dili la shilingi milioni 180, baada ya ujumbe huo nilipokea
simu ya waziri huyo ambaye aliniambia nikifanikisha nitalipwa fedha hizo,”
alisema.
Alisema kuwa
Masele alimtaka aeleze helikopta hiyo itatua wapi, muda gani na kama kweli
wahusika wamo ndani yake kisha ulipuaji ufanywe na watu walioandaliwa.
Alisema
alijiandaa na kufuatilia ila hofu ya kimungu ilimuingia akahofia taifa
litapokeaje tukio la kifo cha Dk. Slaa na yeye akihusika.
“Nilimweleza
Masele lakini alimpigia simu mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna Rose Nyamubi,
ambaye alimshauri kuwa sio vyema tukio hilo likafanyika wilayani kwake, baadaye
nilikutanishwa na katibu mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus
Mapunda pamoja na mtu mmoja wa usalama, ” alisema.
Aidha,
alisema aliwashauri badala ya kulipua watumie mabango na kurubuni vijana
kuhujumu ziara ya Dk. Slaa ambapo walifanikisha hilo.
Alisema
baadaye walikutana tena na Nape, Nchemba na kuombwa wawashawishi madiwani na
viongozi wengine wahamie CCM kwa ahadi ya kupewa ukatibu wa Wilaya kwenye
wilaya watakazoamua.
Alisema
baadaye madiwani hao walienda Mwanza mjini ambapo huko walikutana na Nape
ambaye alieleza kusikitishwa kitendo cha Chadema kumvua uwanachama
Zitto.
KUONDOKA
CHADEMA.
Alisema
Februari 26, mwaka huu waliondoka rasmi Chadema ambapo Nape alifika huko
na kukutana naye hoteli ya Kalena ambapo katika mazungumzo alimhakikishia
maisha mazuri pamoja na uongozi.
“Usiku
ulipofika gari la mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza iliwachukua na kuwapeleka uwanja
wa ndege na kusafiri kuja Dar es Salaam kukutana na Nchemba ambaye naye
aliwataka waelekee Dodoma na baadaye Kalenga,” alisema.
Aliongeza
kuwa Dodoma walienda nyumbani kwa Kinana ambaye huko waliwakuta
Masele, Nchemba na Mchange ambapo wakati wote Katibu Mkuu alisifu
kitendo chao cha kuondoka Chadema.
Alisema
katika mazungumzo makada hao walimwambia Nchange asichoke kwa kazi anayofanya.
CHAMA CHA ACT
CHATAJWA .
Mzuka
alisema makada hao walikubaliana mgogoro ndani ya Chadema lazima uboreshwe na
kuahidi kugharamia fedha za kwenda mikoani na pia wakasema kuna chama
kitasajiliwa.
Pia alisema
makada hao walisema watahakikisha Msajili wa vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi anakipatia usajili wa kudumu kwa gharama yoyote chama cha ACT ili CCM
ipate ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema
katika mazungumzo hayo, Kinana alisema ACT imeanzishwa kwa lengo maalum
la kuipa CCM ushindi kwa kuwa hata huko duniani, ushindi wa chama tawala
unatokana na usajili wa vyama vipya.
WABUNGE
WANNE KUHUJUMIWA.
Tundu Lissu. |
Makada hao
walikubaliana katika uchaguzi ujao mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,
asirudi bungeni kwa sababu ameitia hasara serikali kuhusu hoja zake dhidi ya
katiba.
Diwani huyo
alitaja wabunge wengine ambao wapo kwenye mtego huo kuwa ni mbunge wa
Arusha mjini, Godbless Lema ambaye imeelezwa amesababisha kushuka kwa utalii.
Wengine ni
mbunge wa Iringa mjini Mchugaji Peter Msigwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph
Mbilinyi.
Kwa upande
wa Lissu alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Diwani
akijiuzulu anatakiwa aandike barua rasmi kwa mwenyekiti wa Halmashauri na
kuambatanisha na kiapo.
“Hawa
hawakufanya hivyo kwa hiyo bado ni madiwani wa halmashauri ya mji wa
Shinyanga,na uthibitisho kuwa hawajajiuzulu ni kuwa siku 90 zimepita bila
kutangazwa uchaguzi, “ alisema.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
No comments:
Post a Comment