Watanzania
ni mabingwa wa kukosoa, mabingwa wa kujua vitu vizuri kwa wakati, lakini tatizo
zaidi ni kwamba, hawa wanaoongea, siku moja waite waweke kwenye viti na wape
nafasi ya kufanya hili wanaowalalamikia.
Hapo kinaweza kutoka kitu cha ajabu
mpaka ukabaki unajiuliza, waliokuwa wakilalamika ndiyo hawa kweli niliowapa
nafasi, au walikuwa wanatumwa na mtu anayejua na wao walikuwa wasemaji tu?
Somo
langu kubwa na zuri ninalotaka mlielewe ndugu zangu kwa leo ni kwamba, si kila
anayeongea sana anajua kutenda.
Kutenda na kuongea ni vipaji viwili tofauti,
ambavyo viko vichwani mwa watu wawili tofauti.
Tafakari
zaidi, kisha ukimaliza, hatua zinakusubiri.
|
No comments:
Post a Comment