TANGAZO.
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WOTE WANAOTAKIWA
KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWEZI SEPTEMBA KUWA WANATAKIWA
KURIPOTI VIKOSINI TAREHE 13 SEPTEMBA 2014 BADALA YA TAREHE 04 SEPTEMBA 2014.
VIJANA WANAOTAKIWA KURIPOTI NI KAMA IFUATAVYO:-
1. WALIMU WOTE NGAZI YA CHETI (GATCE) 2014. (WALIOMALIZA 2014).
2. WALIMU ELFU TATU NGAZI YA DIPLOMA (DSEE) (WALIOMALIZA 2014).
3. VIJANA WA KIDATO CHA SITA AMBAO
HAWAJAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KUAHIRISHA KAMA ILIVYOTOLEWA MAELEKEZO YA AWALI.
AIDHA JKT LINAKANUSHA UVUMI UNAOENEZWA KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI WA MANENO
"SMS" NA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA VIJANA WA KIDATO CHA SITA
WANAOENDA VYUO VIKUU WANATAKIWA KWANZA KWENDA KWENYE MAKAMBI YA JESHI
KUCHUKUA BARUA ZA KURUHUSIWA KWENDA VYUONI, TAARIFA HIZI SI ZA KWELI BALI NI
UZUSHI NA UPOTOSHAJI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Tangazo Na:-: JKT
|
No comments:
Post a Comment