Tangu mwaka 2011,
tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi
kikubwa cha pesa, na mwaka jana 2013, ikaelezwa kuwa bila Milioni 10 au Milioni
8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya kilichotajwa Agosti 22,2014, kitawapa kizunguzungu zaidi
hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji
huyo.
Kwa mujibu wa Meneja wake Babu Tale, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji
kwa show moja hapa nchini ni Dola elfu 15 (sawa na shilingi Milioni 25 za
Tanzania).
“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi?
Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.” Babu Tale
aliiambia Bongo5.
Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za
nje ya nchi (ikiwemo Marekani).
“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni
zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond
anauza dawa za kulevya.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na Dola
Laki 375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania Milioni 625,687,500).
Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava. |
No comments:
Post a Comment