UFALME WA SOKA ULAYA 2013/2014:-Mtazame Cristiano Ronaldo alivyoifurahia Tuzo yake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 30, 2014

UFALME WA SOKA ULAYA 2013/2014:-Mtazame Cristiano Ronaldo alivyoifurahia Tuzo yake.

Nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa usiku wa Agosti 28,2014 mjini Monaco, Ufaransa.

 Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17 katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia kuisaidia Klabu yake kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.

Ronaldo (katikati) akifurahia baada ya kushinda. 
kushoto ni wachezaji wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi Arjen Robbe kulia.

Cristiano Ronaldo akifurahia na tuzo yake Baada ya kukabidhiwa na alisema: “Nimefurahi kweli kweli. 
Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad