SAKATA LA EMANUEL OKWI KWENDA SIMBA SC:-Soma Kilichofanywa na Yanga SC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 30, 2014

SAKATA LA EMANUEL OKWI KWENDA SIMBA SC:-Soma Kilichofanywa na Yanga SC.


Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari Jana Agosti 29,2014. Kushoto Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.

Klabu ya Yanga imekana kumpa barua Emmanuel Okwi ya kuvunja naye Mkataba na imesema mshambuliaji huyo Mganda, amewahadaa Simba SC ambao wameingia mkenge wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Yanga SC imeandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiiomba ifanye mambo mawili- 1- imfungie Okwi kucheza soka na 2- iifungie Simba SC.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa jana Agosti 29,2014, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amesema kwamba anaipa TFF siku saba kutekeleza hayo.

Manji amesema, iwapo TFF itashindwa kutekeleza hayo ndani ya siku hizo saba, wao watahamia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambako kama hawatafanikiwa pia, watahamia Mahama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).

Manji amesema asubuhi wametuma malalamiko yao kimaandishi TFF na pia wanamdai Okwi fidia ya dola za Kimarekani 500,000 (Sh. Milioni 900) kutokana na kuvunja mkataba na wao.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba, kabla ya jana katika malalamiko ya awali waliyotuma TFF, walitaka Okwi awalipe dola 200,000 (zaidi ya Sh. Milioni 340,000), lakini baada ya Simba kutangaza imemsajili Agosti 28,2014, dau limepanda.

Manji amesema kwamba Yanga haina ubaya na Simba, bali watani wao hao wa jadi, wamefanya vibaya kumsainisha mchezaji huyo bila kuwasiliana nao. 

Pichani Ni Emanuel Okwi akiwa na Hans Poppe wakati anarejea Simba SC.

Juzi Agosti 28,2014, Okwi ametangaza kurejea Simba SC kwa mkataba huru wa muda, akida Yanga SC imempa barua ya kusitisha mkataba naye pamoja na kumshitaki TFF.

Okwi alisema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.

Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”alisema Poppe.

Hapo juu ni Ukurasa wa kwanza  wa Barua ambayo Klabu ya Yanga SC ilitaka mkataba wake na EMMANUEL OKWI Uvunje au Kupunguzwa zoezi  hilo hata hivyo halikufanyika.Chini ni ukurasa unaoendelea wa barua hiyo.


Barua ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF Kuwaita pamoja.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad