Leo Agosti
27,2014,Usiku, Arsenal wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya
Uturuki Besiktas kwenye Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI 2014/2015.
Wiki
iliyopita huko Instanbul, Besiktas na Arsenal zilitoka 0-0 na Arsenal
wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli itamaanisha
Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Droo
yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi Agosti 28,2014.
Arsenal
wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae alipewa
Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul.
Pia Arsenal
itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na vile vile kumkosa
Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.
Kukosekana
kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo au Lukas Podolski au
hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama Sentafowadi au ikibidi, Arsene Wenger
kumtumia Joel Campbell.
Wakati
Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena
Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya
zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia
kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza
na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.
**Mechi
zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku**Kwenye
Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza.
Jumatano
Agosti 27,2014.
Arsenal v Besiktas [0-0]
Athletic Bilbao v Napoli [1-1]
Bayer 04 Leverkusen v FC Copenhagen [3-2]
Ludogorets Razgrad v Steaua Bucharest [0-1]
Malmö FF v FC Red Bull Salzburg [1-2]
|
No comments:
Post a Comment