Mkutano huo
mkuu wa Wanataaluma wanaotoka Ngara NDUGSO ulikutana na Wanachama wote na Wadau
wa Maendeleo wilayani Ngara mkoani Kagera
Agost 09,2014 katika Ukumbi wa Ngara Sekondari ambapo Katibu mkuu wa
NDUGSO Bw.Herberth amesema Lengo la mkutano huo pamoja na mambo mengine
waliibuka na Maazimio yaliyoilenga wilaya ya Ngara lakini pia kuuhusu umoja huu wa NDUGSO
ambayo ni:-
- Kuwa mwaka huu 2014,Umoja uyafikie maeneo ya
zilipokuwa kambi za Wakimbizi ili kupeleka elimu, utashi na uhiari katika
kupanda miti ili kutunza mazingra, lakini pia kikao kiliazima kuomba ardhi kwa
mamlaka husika ili kupanda miti ya mfano kwa jamii katika kuihamasisha jamii
juu ya utunzaji mazingira.
- Kuhusu Uchimbaji
wa Kabanga Nikel, Meneja mahusiano ya jamii wa Mgodi huo uliopo wilayani Ngara,alituhabarisha
kuwa mradi wa Kabanga Nickel umesimama kwa muda sababu ya kuporomoka kwa bei ya
nikel ktk soko la Dunia.
|
No comments:
Post a Comment