UBINGWA WA SUPER CUP 2014:-Hivi ndivyo Ronaldo aiongoza Real Madrid kuichapa Seville bao 2-0 Uwanja wa Cardiff City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 13, 2014

UBINGWA WA SUPER CUP 2014:-Hivi ndivyo Ronaldo aiongoza Real Madrid kuichapa Seville bao 2-0 Uwanja wa Cardiff City.

Mchezaji bora wa Dunia,Cristiano Ronaldo amefunga mabao yote mawili yaliyoipa ushindi wa mabao 2-0 timu yake ya Real Madrid dhidi ya FC Seville kwenye mchezo wa UEFA Super Cup uliopigwa nyumbani kwa Gareth Bale Mjini Cardiff kwenye dimba la Millenium.

 Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao hayo mbele ya mashabiki 33,500 na kuipa Real Madrid Ubingwa huo kwa mara nyingine tangu mwaka 2002.

Mchezo huo pia ulihudhuliwa na kocha wa zamani wa Man Utd Sir Alex Ferguson.
Nahodha wa timu hiyo Iker Casillas alikaa milingotini siku moja tu baada ya aliyekuwa mpinzani wake msimu uliopita Diego Lopez kujiunga na AC Milan ya Italia.

Kikosi kipya cha kwanza cha Real Madrid kilichotwaa Super Cup Jana Usiku (Agosti 12,2014) ambapo Real Madrid kwenye mchezo huo iliwatumia nyota wake iliowasajili msimu huu kiungo mjerumani Toni Kroos pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina James Rodriguez.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad