Michuano ya kombe la Kagame linaloendelea
nchini Rwanda imeendelea kushika kasi ambapo Leo hii Agosti 12,2014, klabu
bingwa ya Tanzania Azam FC ilijitupa dimbani kwa mara 3 kwa kucheza dhidi ya
Atlabara ya Sudan Kusini.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya 2-2, huku
mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, mburundi Didier Kavumbagu akiinusuru Azam
kupata kipigo baada ya kuisawazishia Azam dakika ya 86, baada ya krosi ya
Shomary Kapombe.
Azam ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa
bao 1-0 lililofungwa na kiungo Kipre Michael Balou kwa shuti la mpira wa adhabu
kutoka umbali wa mita 20, baada ya pacha wake, Kipre Herman Tchetche
kuangushwa.
Atlabara ilirudi vizuri kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao dakika
ya 48, mfungaji Nahodha wake, Thomas Batista kabla ya kufunga la pili dakika ya
60 mfungaji Bony Martin.
Atlabara ilipata pigo dakika ya 89 baada ya Nahodha wake, Batista kutolewa nje
kwa kadi nyekundu.
Kwa matokeo hayo, Azam FC
inafikisha pointi 5 baada ya mechi tatu na kujihakikishia nafasi ya kwenda Robo
Fainali ya michuano hiyo, wakati Atlabara inafikisha pointi 2 baada ya mechi
mbili.
|
No comments:
Post a Comment