Watu 16
wamefariki papo hapo baada ya Mabasi mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana
uso kwa uso kwenye kijiji cha Morogoro wilayani Sikonge Mkoani Tabora
Taarifa ya Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Bi Suzan Kaganda amesema ajali hiyo iliyotokea jana Agosti
19,2014, majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili ya Kampuni ya SABENA lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Mkoani
Tabora pamoja na basi la AM Coach lililokuwa likitokea Mwanza kwenda wilayani
Mpanda Mkoani Katavi.
Amesema
waliotambuliwa ni 10 wakiwemo madereva wa magari hayo ambao ni Aristedis
Shirima wa Basi la AM Coach na James Komba wa Basi la SABENA.
Mabasi hayo ya
AM Coach na SABENA yamepata ajali ambapo
chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo,majeruhi
wamelazwa kwenye hosptali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ambao jumla yao ni
75,waliopoteza maisha jumla 17 na 10 wametambuliwa.
Aidha mmoja
wa majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Christopher amesema ajali hiyo
imesababishwa na vumbi kubwa lililotokea baada ya kupishana na gari jingine.
Kamanda
Kaganda amewataka watu kwenda katika Hospitali ya wilaya ya Sikonge kwa ajili
ya utambuzi wa marehemu waliobaki.
|
No comments:
Post a Comment