LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya mechi zote za Agosti 23,2014 ukiwemo wa Chelsea v/s Leicester - Everton v/s Arsenal . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 23, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya mechi zote za Agosti 23,2014 ukiwemo wa Chelsea v/s Leicester - Everton v/s Arsenal .

Diego Costa ameendelea kung'ara Chelsea akifunga katika ushindi wa 2-0 leo Agosti 23,2014.  

 The Blues wanashinda mechi ya pili mfululizo Ligi Kuu ya Uingereza 2014/2015 kwa kuichapa Leicester City mabao 2-0 Uwanja Stamford Bridge.

Costa alifunga bao la kwanza dakika ya 62, kabla ya Eden Hazard kufunga la pili dakika ya 77.

RAHA YA USHINDI:-Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Oscar/Willian dk70, Hazard, Schurrle/Ramires dk64 na Costa/Drogba dk80.

Leicester City; Schmeichel, De Laet, Konchesky, Morgan, Hammond/Taylor-Fletcher dk73, King, Schlupp, Mahrez/Albrighton dk68, Nugent na Ulloa/Wood dk84.


Diego Costa alimpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 80 huku akipigiwa makofi wakati anatoka nje.

Nao Arsenal, wakiwa Ugenini huko Goodison Park, walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Everton huku Bao lao la Pili likifungwa mwishoni katika dakika za Majeruhi.

Huku wakikumbuka kichapo cha hapo hapo Goodison Park Mwezi Aprili walipopigwa Bao 3-0 na Everton, Arsenal walijikuta wako Bao 2-0 nyuma hadi Mapumziko.

Bao la kwanza la Everton lilifungwa na Fulbeki Seamus Coleman kwa kichwa katika Dakika ya 19 baada ya kazi safi ya Gareth Barry.

Bao la pili kwa Everton lilipatikana Dakika ya 45 baada Romelu Lukaku kuwachambua Mabeki wa Arsenal, Per Mertesacker na Monreal, na kumpasia Steven Naismith aliepiga Shuti la chini na kumpita Kipa Wojciech Szczesny.

Arsenal walianza Kipindi cha Pili kwa kumwingiza Olivier Groud badala ya Mchezaji wao mpya Alexis Sanchez ambae katika Kipindi cha Kwanza chote, akicheza kama Sentafowadi, alishindwa kuingia kwenye boksi hata mara moja.

Kipindi cha Pili, Arsenal walijitutumua lakini Everton walijizatiti sana kulinda Bao zao lakini baada ya Arsenal kufanya mabadiliko kwa kuwaingiza Santi Cazorla na Joel Campbell badala ya Wilshere na Oxlade-Chamberlain kidogo uhai ulipatikana.

Arsenal wakafunga Bao lao la kwanza Dakika ya 83 kupitia Aaron Ramsey kufuatia kazi nzuri ya Santi Cazorla na kusawazisha katika Dakika za Majeruhi kwa Bao la Olivier Giroud.

Matokeo mengine yapo kama ifuatavyo: -Jumamosi Agosti 23,2014.

Aston Villa 0 – 0 Newcastle 

Crystal Palace 1 – 3 West Ham 

Southampton 0 – 0 West Brom 

Swansea 1 – 0 Burnley 

Everton 2 Arsenal 2

As It Stands Table


Position Team Played Goal Difference Points

Jumapili Agosti 24,2014.

1530 Hull v Stoke

1530 Tottenham v QPR

1800 Sunderland v Man United

Jumatatu Agosti 25,2014.

2200 Man City v Liverpool

Jumamosi Agosti 30,2014.

1445 Burnley v Man United

1700 Man City v Stoke

1700 Newcastle v Crystal Palace

1700 QPR v Sunderland

1700 Swansea v West Brom

1700 West Ham v Southampton

1930 Everton v Chelsea

Jumapili Agosti 31,2014.

1530 Aston Villa v Hull

1800 Leicester v Arsenal

No Movement 1 Chelsea 2 4 6
Moving up 2 Swansea 2 2 6
No Movement 3 Arsenal 2 1 4
Moving up 4 Aston Villa 2 1 4
Moving down 5 Man City 1 2 3
Moving up 6 West Ham 2 1 3
Moving down 7 Liverpool 1 1 3
Moving down 8 Hull 1 1 3
Moving down 9 Tottenham 1 1 3
Moving down 10 Everton 2 0 2
Moving up 11 West Brom 2 0 2
Moving down 12 Sunderland 1 0 1
Moving up 13 Southampton 2 -1 1
Moving down 14 Leicester 2 -2 1
Moving up 15 Newcastle 2 -2 1
Moving down 16 Man Utd 1 -1 0
Moving down 17 QPR 1 -1 0
Moving down 18 Stoke 1 -1 0
Moving down 19 Crystal Palace 2 -3 0
Moving down 20 Burnley 2 -3 0

KIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad