SHERIA:- Wakazi wawili wa kijiji cha Muruvyagira wilayani Ngara Mkoani Kagera wamefikishwa Mahakamani kwa mauaji ya wanandoa wawili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 14, 2014

SHERIA:- Wakazi wawili wa kijiji cha Muruvyagira wilayani Ngara Mkoani Kagera wamefikishwa Mahakamani kwa mauaji ya wanandoa wawili.

Wakazi wawili wa kijiji cha Muruvyagira wilayani Ngara Mkoani Kagera wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo wakituhumiwa kwa mauaji ya wanandoa wawili yaliyotokea Agosti 07,2014, kijijini humo.

 Mbele ya Hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Bw Andrew Kabuka, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw Stividana Webiro amewataja washitakiwa kuwa ni Ayoub Mathias na Philmon Matoni wanaotuhumiwa kumuua Bw Jackson Ntibulikule na Bi Jeniroza Jackson kwa kuwakata mapanga.

Hata hivyo washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi ya mauaji ambapo wamerudishwa rumande hadi Agosti 27 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

Wakati huo huo Kijana Mathias Davis mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa Murugwanza Wilayani Ngara amefikishwa katika mahakama hiyo akishitakiwa kwa kujaribu kujinyonga

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alifanya tukio hilo August 11 mwaka huu kaatika eneo la Murugwanza ambapo hata hivyo amekanusha shitaka hilo na kesi yake imeahirishwa hadi Agosti 27 mwaka huu.

 Habari Na:-Radio Kwizera FM-Ngara.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad