AJALI:-Pikipiki yanasa chini ya Lori la mafuta baada ya Kugongana huku Mtu mmoja Akifariki papo hapo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 14, 2014

AJALI:-Pikipiki yanasa chini ya Lori la mafuta baada ya Kugongana huku Mtu mmoja Akifariki papo hapo.

Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso .

Ajali imetokea barabara kuu ya Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Sacania lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).

Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya Lori la mafuta.

Mashuhuda wa ajali hiyo waliuambia mtandao huu  kuwa ilitokea majira ya saa 7 katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo chuo cha Polisi Moshi kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.
 
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo Katika ajali hiyo Mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya, mfanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, alifariki dunia papo hapo. ..Na Dixon Busagaga 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad