Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa
Viongozi wa Nchi 50 kutoka Afrika na Marekani ambao umewakutanisha na
Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC
Agost 6, 2014…
Viongozi hao wa Afrika walikuwa na mazungumzo mjini Washington jumatano Agost
06,2014, kuhusu kupanua biashara, kuimarisha usalama na kuboresha
uwajibikaji wa serikali kote barani Afrika.
Mazungumzo
hayo ni katika mifululizo ya mikutano iliyofanyika ikiwa ni kilele cha mkutano mkubwa wa siku tatu
unaowashirikisha wakuu wa mataifa 50 kutoka barani Afrika. Katika matamshi yake
ya ufunguzi hapo jumatano, Rais Obama alisema Afrika mpya inajitokeza. “Huku
baadhi ya chumi zikikua haraka sana duniani, ukuaji wa daraja la kati na vijana
na ukuaji wa haraka sana wa idadi ya watu duniani, Afrika itasaidia kujenga
muundo wa dunia ambao haujawahi kuwepo awali”.
Rais
alisema kuongezeka fursa za biashara barani Afrika kutasaidia kuandaa uhusiano
kati ya Marekani na bara la Afrika.
Rais Obama ametangaza dola bilioni 33 katika
uwekezaji binafsi na wa umma nchini Marekani kwa mataifa mbali mbali barani
Afrika.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
|
Rais Barack
Obama wa Marekani, amesema nchi yake itayasaidia mataifa ya Afrika kuunda
kikosi cha dharura kitakachovisaidia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika.
Akihitimisha
mkutano kati yake na viongozi wa nchi 50 wa Afrika mjini Washington, Rais Obama
amesema kikosi hicho kinaweza kupelekwa haraka kuvisaidia vikosi vinavyoungwa
mkono na Umoja wa Mataifa barani Afrika.
Amesema nchi
sita zitakazohusishwa katika kuimarisha usalama wa Afrika ni pamoja na Ghana,
Rwanda, Senegal, Tanzania, Ethiopia na Uganda.
Taarifa ya
Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa nchi hiyo itatumia Dola milioni 110 kwa mwaka
katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano, kusaidia kuundwa kwa kikosi kipya.
Hata hivyo,
Rais Obama hakufafanua ni vipi kikosi hiko cha kulinda amani kitakavyohusiana
na vikosi vya sasa vya Umoja wa Afrika.
Hapo jana, Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani, Kerry aliwaonya viongozi hao kwamba makundi ya
siasa kali ni kitisho kikubwa kwa uchumi unaokuwa barani Afrika, kwani
yanawalenga vijana wengi wasiokuwa na ajira.
Kerry
alisema kwamba idadi ya watu milioni 700 wenye umri wa chini ya miaka 30
walioko Afrika, haijawahi kukutikana popote pale kwenye historia ya ulimwengu,
na hivyo ni wajibu wa viongozi wa Afrika kulilinda kundi hilo lisiangukie
mikononi mwa makundi kama vile Boko Haram la Nigeria na al-Shabaab la Somalia.
Habari Na:-DW Swahili.
No comments:
Post a Comment