Shirika la
afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika
kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura.
WHO imesema
kuwa mataifa yalio na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa
kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa
kimataifa.
Tangazo hilo
linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Geneva kuhusu uwezekano wa kutuma
wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari
zaidi.
Ugonjwa huo
umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika .
Mataifa
yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia visa
vimeripotiwa nchini Nigeria.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
No comments:
Post a Comment