Picha juu na chini ni Madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kilichofanyika Agost 05,2014,katika ukumbi wa Halmshauri hiyo . |
Baraza la Madiwani wa halmashauri ya
wilaya ya Ngara mkoani kagera jana limetangaza
kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Colnery
Ngudungi kwa kushindwa kutekeleza
maagizo ya kumchukulia hatua aliyekuwa
Meneja wa Mamlaka ya maji mjini Ngara Bw.Edward Magai kwa kufuja fedha zaidi ya Sh 32 milioni.
Wakichangia hoja ya ubadhilifu wa fedha alizotoa Rais
kikwete kwa mamlaka ya mji mdogo wa Ngara kiasi cha Sh 200 milion huku kiasi kilichokwisha pokelewa ni Sh 150 milioni ,ambapo Madiwani hao wameonesha kusikitisha na utekelezaji wake kusuasua huku hakuna juhudi zinazoonekana katika matumizi ya fedha hizo.
Diwani wa Kata
Mulukulazo,Bw. Mukiza Byamungu amesema atafungua kesi mahakamani dhidi ya
viongozi wa halmashauri hiyo kwa kuendelea kumkumbatia meneja huyo ambaye
amefuja fedha hizo na ameshastaafu.
Naye Diwani wa Kata ya Ntobeye Bw.John
Ruzige amesema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa namna moja ama nyingine
anahusika na kupotea kwa fedha hizo kwani kila kunapokuwa na kikao chenye hoja
za maji na changamoto za halmashauri hukwepa kikao nakukaimisha mkuu wa idara.
Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na
kanuni za utumishi, mfanyakazi anapoacha ma kustaafu kiutumishi anastahili
kukabidhi nyaraka mbali mbali lakini Bw.Edward Magai hajakabidhi mali za
halmashauri wala nyaraka za serikali.
Amesema fedha kutoka ofisi ya
Rais ni kiasi cha jumla ya Sh 150 milioni na kati ya fedha hizo Sh 37 milioni
zimetumika kununua vipuli vipya vya
kufunga mitambo ya kusukuma maji na kiasi kingine kilichobaki hakikufanya jambo
lililokusudiwa la kuwapatia wananchi huduma ya maji .
Aidha Diwani wa Mamlaka ya mji ndogo wa Ngara,Bw.
Charles Rujuba amesema kuna haja ya kuitisha kikao cha
baraza la dharula ndani ya siku saba kutaka mkurugenzi wa
halmashauri hiyo kutoa maelezo juu ya suala hilo.
“Katika mamlaka ya maji mjini ngara
meneja aliyeshika nafasi hiyo hana vitendea
kazi kwa kuwa kabati zimefungwa na
meneja aliyestaafu Magai amejimilikisha
funguo na kukwamisha shughuli za kijamii”Alisema Rujuba.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Bw Herman Hume amesema
Meneja huyo alipewa siku 10
kujieleza kuhusu matumizi ya fedha hizo lakini hakutekeleza hivyo
anaridhia maoni ya baraza na
atahakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
Katika baraza hilo madiwani
wamemchagua kwa mara nyingine aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo ,Bw. Soud Mkubila
ambaye ataongoza halmashauri ikiwa ni kipindi chake kwa mara ya nne.
Wajumbe wengine wa kamati waliochaguliwa ni Mwenyekiti kamati
ya Elimu,Afya, na Maji (Willibard Bambara), Kamati ya
Uchumi,Ujenzi na Mazingira ( John
Ruzige) na kamati ya Maadili ya wilaya ni Bw.
Tomson Seyongwe.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
No comments:
Post a Comment