Mke wa
zamani wa hayati Nelson Mandela, anataka watoto wake wapewe nyumba ya marehemu
iliyoko kijijini Qunu.
Hatua hiyo
huenda ikazua mgogoro wa kwanza wa kisheria kuhusiana na mali ya hayati Mandela
tangu kuaga dunia mwaka 2013.
Mawakili wa
Winnie Madikizela-Mandela wamesema kudai nyumba hiyo ni haki yake ya kitamaduni
kwani aliwahi kuwa mke wa hayati Mandela.
Mali ya
hayati Mandela ilikadiriwa kuwa yenye thamani ya dola milioni 4.3 baada ya kifo
chake mwezi Disemba mwaka 2013.
Mzee Mandela
alimpa talaka bi Madikizela-Mandela mwaka 1996.
Wawili hao
walifanikiwa kupata watoto wawili, Zinzi na Zenani.
Hayati
Mandela ana mtoto mmoja kwa jina Makaziwe kutoka kwa ndoa yake ya kwanza kwa
marehemu Evelyn Mase.
Wakati wa
kifo chake alikuwa amemuoa,Graca Machel, mkewe marehemu Samora Machel,
aliyekuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji.
.......Bi.Winnie
Mandela anataka nyumba ya marehemu Mandela ikabidhiwe wanawe...
|
'Mila na
Tamaduni'
Katika wasia
wake, marehemu Mandela alisema: ''Mali yake ya Qunu ikiwemo nyumba hiyo
inapaswa kutumiwa na familia yake nzima ili kukuza umoja katika familia hiyo ''
Katika barua
hiyo ambayo BBC imeweza kuiona, mawakili walisema kuwa Bi Madikizela-Mandela
ndiye alipata nyumba hiyo katika eneo la Qunu, wakati Mandela alipokuwa
generezani akipigana dhidi ya utawala wa mzungu.
''Msimamo
wetu ni kwamba nyumba hiyo ni mali ya kizazi cha Mandela na Winnie
Madikizela-Mandela,'' ilisema barua hiyo.
''Ni katika
nyumba hii pekee ambapo watoto na wajukuu wa Madikizela-Mandela wanaweza
kuendesha shughuli zao, na nyumba hiyo haiwezi kukabidhiwa kwa mtu yeyote
ambaye sio mtoto wala mjukuu wake. ''
Barua hiyo
ilisema kuwa haimaanishi kwamba watoto wengine wa Mandela watanyimwa ruhusa ya
kuingia katika nyumba hiyo.
"lakini
udhibiti na usimamizi wa nyumba unapaswa kufafanuliwa kwa misingi ya kitamaduni
na mila,'' walisema mawakili hao.
Simanzi
ilitanda kote duniani kufuatia kifo cha Mandela mwaka 2013 akiwa na umri wa
miaka 95.
Alisifika
kwa kupigana dhidi ya utawala wa wuzungu na kwa rais wa kwanza mzalendo wa
Afrika Kusini baada ya kutoka jela ambako alifungwa kwa miaka 27.
Habari na :-BBC Swahili.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
No comments:
Post a Comment