UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana(Agost
04,2014) walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika
mjadala uliofanyika Dar es Salaam kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu
kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na
wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe
wenzake, Profesa Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu
Malale na Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba
lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana(Agost 04,2014.
Jaji Warioba ndiye alianza
kuzungumza kwa kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa
amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana
ukweli bali maoni aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi
waliyokusanya wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza
kusaidia katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi(Agost 03,2014), katika
mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), William Lukuvi alidai kuwa Jaji Warioba amewasilisha
serikalini maoni mapya, ukiacha yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume
iliandaa sura ya kwanza iliyohusu mali na maliasili na sura ya tano kuhusu
Serikali ya Muungano na sura ya nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki
nazo lakini Machi 27, mwaka huu niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na
Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani,
Mathias Chikawe) kwa kuwa alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi hicho na
nikawakabidhi ili isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati wa kuandaa
Katiba ya Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo
mapya wala sikupeleka mawazo mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa
wananchi na nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi
na mimi nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie kujua
wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua
sababu za tume kupendekeza muundo wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo
kutokana na idadi ya watu waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja
zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya
watu waliotaka muundo wa serikali tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo
kwa sababu ya hoja zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,”
alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni
Tanganyika kuvaa koti la Muungano pia akifafanua jinsi Tanzania Bara
inavyoshughulikia masuala yake ya kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande
wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa
muungano wanaotembelea Zanzibar kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna
mgongano wa Katiba ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo
limekuwa na mvutano kwa muda mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti
ya pamoja,” alisema na kuongeza.
No comments:
Post a Comment